Friday, December 20, 2013

Bado natafuta yaendelea kutesa sokoni

Shamsa Ford, amefanya mambo makubwa sana humo ndani
Kwa niaba ya crew nzima ya Jerusalem Film Company, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kabisa kwa mamilioni ya mashabiki wetu ambao mmeendelea kutuunga mkono na kutupa nguvu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii kubwa ili kuzalisha filamu ambazo zitawakonga nyoyo zenu sanjari na kuwaelimisha.

Takriban wiki sasa toka filamu ya "Bado Natafuta" kuingia rasmi sokoni, tumekuwa tukipokea maoni toka kwa wadau na mashabiki wetu karibu kila kona, hali ambayo inatuaminisha kuwa kazi yetu mmeikubali na mnatuunga mkono kwa kuinunua kwa wingi.

Ikiwa hujabahatika kupata nakala yako halisi hadi sasa au unapata tatizo la namna ya kuipata, tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano hapo juu, nasi tutakuelekeza kitu cha kufanya ili uweze kumiliki nakala yako halisi.

Asanteni sana kwa kutuunga mkono

Tags: ,

0 Responses to “Bado natafuta yaendelea kutesa sokoni”

Jisajili Kupata Habari Mpya

Ikiwa ungependa kupata taarifa zetu mara kwa mara, pindi tu zinapowekwa hapa, jisajili kwa kuandika anwani ya barua pepe hapa chini kisha fuata maelekezo

© 2013 Jerusalem Film Company. All rights reserved.
BlogTheme Edited by Rama Msangi