Friday, December 20, 2013

Inasubiriwa kwa hamu sana .... DANIJA

Ikiwa takriban wiki moja sasa toka mzigo wetu mpya unaokwenda kwa jina la "Bado Natafuta uingie madukani, tumeendelea kupokea ujumbe na simu kutoka kwa mashabiki wetu waliosambaa sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, wakiulizia ni lini filamu ya DANIJA itaingia madukani.

Ikumbukwe kuwa, filamu hizi mbili zilikuwa zikitangazwa kwa pamoja, na ni wazi mashabiki wetu wengi walitarajia kuwa huenda zingetoka kwa pamoja, lakini kumbe haijawa hivyo. 

Tunapenda kuwashukuru kwani hii yote imekuwa ikionyesha kiasi gani mnatupa support ya kutosha na kutuhamasisha kuendelea kufanya kazi kwa minajili ya kuwapatia furaha ambayo mnaitarajia toka kwenye kazi zetu. Na kupitia taarifa hii, tunapenda pia kuwaeleza kuwa, filamu ya DANIJA haijaingia rasmi sokoni, ingali iko kwenye hatua za mwisho za kuingizwa sokoni na panap[o majaaliwa, mwezi januari itakuwa sokoni.

Ikiwa kuna shabiki yetu yeyote ambaye labda amekuwa akisikia kuwa filamu hii iko madukani, au akabahatika kuiona mahali, tunaomba awasiliane nasi haraka kwani hiyo si nakala halali ya kazi yetu kwasababu kazi yetu bado haijaingia sokoni.

Tunawashukuru kwa kuzidi kutuunga mkono na wakati tunaendelea kuisubiri, hapa ni sehemu tu ya uhindo utakaokuwa ukipatikana humo

Tags: , ,

0 Responses to “Inasubiriwa kwa hamu sana .... DANIJA”

Jisajili Kupata Habari Mpya

Ikiwa ungependa kupata taarifa zetu mara kwa mara, pindi tu zinapowekwa hapa, jisajili kwa kuandika anwani ya barua pepe hapa chini kisha fuata maelekezo

© 2013 Jerusalem Film Company. All rights reserved.
BlogTheme Edited by Rama Msangi