Recent Articles
Showing posts with label video. Show all posts
Showing posts with label video. Show all posts

Monday, December 30, 2013

Video: DANIJA IPO MTAANI.......PATA NAKALA YAKO!

Monday, December 30, 2013 - by Unknown · - 0 Comments


JB mwenyewe na wakali wengine kibao utawapannda ndani ya filamu mpya ya DANIJA

Hakikisha unapata nakala halisi ya filamu hii nzuri sana kutoka Jerusalem Film Company.



Tuesday, December 24, 2013

WAGENI WANGU............ Coming Soon!!

Tuesday, December 24, 2013 - by Unknown · - 0 Comments

Bi Staa kama anavyojulikana na wengi....

Pata uhondo kwa muhtasari......mambo kamili yaja endelea kutembelea blog yetu!!



Saturday, December 21, 2013

(Video) TANGLED MESS aka GUILTY by Cassie Kabwita!!

Saturday, December 21, 2013 - by Unknown · - 0 Comments




Baadhi ya vipande kwenye harusi ya Hemed na Cassie ( Kwenye filamu ) itakayojulikana kama Tangled Mess au Guilty.
Pata uhondo!!!

Friday, December 20, 2013

VIDEO: Utambulisho wa Mikono Salama

Friday, December 20, 2013 - by Unknown · - 0 Comments

Jokate, Jacob Stephen, Irene Uwoya, Single Mtambalike, Adam Kuambiana, Stela Mjata, Mzee Ibrahim, Hashim Kambi na Bi Star...hebu tuache masihara jamani, kuna jina la star gani ambalo halipo hapo? Kuanzia wale wa kizazi kileee, hadi hiki cha sasa?

Vichwa hivi adhimu, vinakutana katika mzigo huu unaokwenda kwa jina la Mikono Salama. Tunajua hali ilivyo katika magereza zetu nyingi nchini, sasa inakuwaje mtu ajihisi yuko salama wakati yuko gerezani? Kwanini hasa iwe hivyo? Onja uhondo hapa wakati unasubiri mzigo kamili kushuka hivi karibuni

Inasubiriwa kwa hamu sana .... DANIJA

- by Unknown · - 0 Comments

Ikiwa takriban wiki moja sasa toka mzigo wetu mpya unaokwenda kwa jina la "Bado Natafuta uingie madukani, tumeendelea kupokea ujumbe na simu kutoka kwa mashabiki wetu waliosambaa sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, wakiulizia ni lini filamu ya DANIJA itaingia madukani.

Ikumbukwe kuwa, filamu hizi mbili zilikuwa zikitangazwa kwa pamoja, na ni wazi mashabiki wetu wengi walitarajia kuwa huenda zingetoka kwa pamoja, lakini kumbe haijawa hivyo. 

Tunapenda kuwashukuru kwani hii yote imekuwa ikionyesha kiasi gani mnatupa support ya kutosha na kutuhamasisha kuendelea kufanya kazi kwa minajili ya kuwapatia furaha ambayo mnaitarajia toka kwenye kazi zetu. Na kupitia taarifa hii, tunapenda pia kuwaeleza kuwa, filamu ya DANIJA haijaingia rasmi sokoni, ingali iko kwenye hatua za mwisho za kuingizwa sokoni na panap[o majaaliwa, mwezi januari itakuwa sokoni.

Ikiwa kuna shabiki yetu yeyote ambaye labda amekuwa akisikia kuwa filamu hii iko madukani, au akabahatika kuiona mahali, tunaomba awasiliane nasi haraka kwani hiyo si nakala halali ya kazi yetu kwasababu kazi yetu bado haijaingia sokoni.

Tunawashukuru kwa kuzidi kutuunga mkono na wakati tunaendelea kuisubiri, hapa ni sehemu tu ya uhindo utakaokuwa ukipatikana humo

Wednesday, December 18, 2013

Siku ya makahaba kuadhimishwa duniani.....

Wednesday, December 18, 2013 - by Unknown · - 0 Comments

Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Makahaba nchini Kenya waandamana kudai haki zao ya kwamba biashara ya ngono itambulike kama biashara nyingine!!!!


Chanzo: KTN

Coming Soon: hukumu ya ndoa yangu

- by Unknown · - 0 Comments

Moja kati ya filamu bomba kutoka Jerusalem Film Company, itakayokuwa mtaani mapema mwaka ujao.Usisubiri kuhadithiwa.......Pata nakala yako mara tu utakaposikia ipo sokoni.

Friday, October 11, 2013

Muendelezo........Senior Bachelor(1) Part4 of 5

Friday, October 11, 2013 - by Unknown · - 0 Comments




Daaah hii scene niliipenda sana yani it was so real.....pata uhondo mdau wangu kama vipi tafuta copy yako ili ufaidi uhondo huu kila siku nyumbani kwako na familia yako....

''Eric Fooord tumemuonaaaa!!!!

VIPANDE VYA VIDEO KWENYE FILAMU YA SENIOR BACHELOR.....

- by Unknown · - 0 Comments




Pata uhondo....

Saturday, October 5, 2013

DANIJA ... kukujia hivi karibuni

Saturday, October 5, 2013 - by Unknown · - 0 Comments

"Anayejua kumega vikubwa, shurti pia ajue na kulima... wakati unanigeuza geuza kama chapati, ulikuwa unakenua meno, ukijiona umefika..." 
Unajua nini chanzo cha haya yote? Na mwisho wake ulikuwa nini? Usiwe na shaka, kwani majibu ya maswali haya yote yapo ndani ya mzigo mpya unaokwenda kwa jina la DANIJA.

Kama ilivyo kawaida yetu, hakuna kuremba. Ni mwendo wa kazi zaidi tukiwa tunatambua kuwa unahitaji nini haswa, na ndio sababu tunapenda kukuweka mkao wa kula kwa ajili ya kushuhudia mambo makubwa ndani ya filamu hii.

COMING SOON: bado natafuta

- by Unknown · - 0 Comments

Moyo wangu ulikuwa mbali lakini uliendelea kutambua uwepo na thamani ya mapenzi yangu kwako. Moyo huu huu uliweza kugusa wa kwako wakati hauna kitu, Na moyo huu huu ndio umerudi tena kwa mara nyingine kukukumbusha mateso uliyapata, Na mateso uliyokuwa unasikia wakati uko mbali na mie
Moyo wangu umekubali kusamehe...

Naam, ni chini ya kampuni mahiri yenye kikosi cha watu wenye kujua nini mashabiki wanapenda, Jerusalem Films Company, hapa akiwepo mwanadada mahiri Shamsa Ford ambaye wala hatuhitajiki kueleza sifa zake maana kila mmoja  anazijua, pale kuna Gabo, Patcho Mwamba na wakali wengine kibao.

Ni katika BADO NATAFUTA. Unajua nini kinatafutwa? Tizama utangulizi wa picha hii hapa kisha ujiandae kwa uhondo uliokamili hivi karibuni

Tuesday, October 1, 2013

VIDEO: Nakwenda kwa Mwanangu... Mkongwe Majuto anapoungana na vijana kufanya mambo makubwa

Tuesday, October 1, 2013 - by Unknown · - 0 Comments

Unaweza kucheka hadi ukalia humu, lakini unadhani watu hawatakiwi kujifunza huku wakiwa wanafurahi? Tizama video ya utambulisho wa filamu hii ya Nakwenda Kwa Mwanangu hapa chini, ujue kuwa ni kiasi gani unakosa mambo makubwa ikiwa bado hujawa nayo katika maktaba yako

FIKRA ZANGU ... pata kuelewa nini kilichomo ndani yake

- by Unknown · - 0 Comments

Fikra Zangu, ni kazi yetu nyingine ambayo kama ilivyo ada, imezingatia sio tu ubora wa kazi bali maadili na mahitaji ya kiburudani ya wapenzi wetu. Kama hujabahatika kuiona, basi ionje kwa kucheki video ya utambulisho hapa chini

VIDEO: utambulisho wa DJ Ben

- by Unknown · - 0 Comments

Ni DJ Ben, ikiwa na wakali kibao kama ilivyo kawaida yetu, wakifanya mambo makubwa yenye kufurahisha na kuelimisha. Kama bado hujabahatika kuitizama, hebu angalia vipande vyake hapa, kisha ujiulize kama kweli unastahili kuikosa hii kitu?

Jisajili Kupata Habari Mpya

Ikiwa ungependa kupata taarifa zetu mara kwa mara, pindi tu zinapowekwa hapa, jisajili kwa kuandika anwani ya barua pepe hapa chini kisha fuata maelekezo

© 2013 Jerusalem Film Company. All rights reserved.
BlogTheme Edited by Rama Msangi