Recent Articles
Wednesday, March 26, 2014
Tar 28/3/2014 Bongo Movie Unit inatarajiwa kutimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa. Windhoek Draught wakiwa ndio wadhamini kwa siku yetu hiyo walituwezesha kupeleka mahitaji mbalimbali kwenye wodi ya kinamama na watoto ya hospitali ya Mwananyamala.Ikumbukwe kuwa kinamama na watoto ndio wateja wakubwa wa filamu zetu.
Angalia picha za yaliyojiri leo kwenye tukio hilo...wasanii wengi walijitokeza kufanikisha zoezi hilo...
Tuesday, January 14, 2014
Saturday, January 11, 2014
Mashindano ya Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula yametambulishwa rasmi kwa wakazi wa jiji la Mwanza katika viwanja vya shule ya msingi Buhongwa..
Waandaaji wa mashindano hayo wakiambatana na Balozi wa kampeni ya Grow Jacob Stephen maarufu kama JB pamoja na Jack Monroe ambaye ni Mwanawavuti kutoka nchini Uingereza walifika viwanjani hapo na kulakiwa na umati wa watu waliokuja viwanjani hapo ili kufahamu zaidi kuhusu Maisha Plus / Mama Shujaa wa Chakula.
Angalia picha za matukio yaliyojiri.........
Jack Monroe na JB |
"Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu, tusikate tamaa", alisema JB. |
Huyu ni Khadija Liganga kutoka shirika lisilo la kiserikali la Kivulini la jijini Mwanza. Khadija amefanya kazi nzuri sana kama mshereheshaji wa shughuli hizi. |
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika viwanja vya shule ya msingi Buhongwa. |
Kikundi cha Ngoma na michezo ya nyoka wakitumbuiza katika uzinduzi wa Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula jijini Mwanza. |
Eluka Kibona ambaye ni Meneja wa kampeni, ushawishi na utetezi kutoka Oxfam akizungumza katika hafla hizo. |
Sharon Mariwa kutoka Oxfam akizungumza katika hafla hiyo |
Teresa Yates, Mratibu wa kitengo cha Haki Jinsia kutoka Oxfam akizungumza katika hafla hizo. |
Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwataka vijana kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuchangamkia fomu za Maisha Plus.. Milioni 25 itatolewa kwa mshindi.. |
Baadhi ya wakina mama waliojitokeza kushiriki shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakipokea fomu kutoka kwa Balozi wa Grow JB. |
Baadhi ya vijana wakipokea fomu za ushiriki wa shindano la Maisha Plus kutoka kwa mwanawavuti Jack Monroe. |
Kutana na Francis Bonda, mojawapo wa waandaaji na wasimamizi wa Mashindano ya Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula. |
Kutana na Jack Monroe, mwanawavuti wa masuala yanayohusu chakula wa www.agirlcalledjack.comkutoka nchini Uingereza. Jack ambaye yuko nchini kwa mwaliko kutoka Oxfam in Tanzania atapata fursa ya kutembelea pamoja na kuandika kuhusu mafanikio pamoja na changamoto wanazokutana nazo wakulima kutoka Tanzania. Akiwa nchini, Jack atakutana na wanachama wa kikundi cha wakulima wa mpunga Ngaya mkoani Shinyanga pamoja na kukutana na washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula waliopita. |
Kutana na Mkamiti Mgawe, Afisa wa utetezi na ushawishi kutoka Oxfam. Mkamiti ametoa wito kwa wakina mama wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wakazi wa Tanzania, kuchukua fomu na kushiriki mashindano haya. Fomu za ushiriki zinaweza kujazwa moja kwa moja kupitia link hii --> http://maishaplus.tv/
CHANZO: Growtanzania Facebook Page
|
Tuesday, January 7, 2014
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwasilisha msaada wa pesa na nguo toka kwa wasamaria wema akina Yassin Kapuya , Hassan Othmani, Mwandishi mwenzetu Othman Michuzi , Pendo Fundisha |
Baadhi ya waandishi wa habari waliomtembelea mama huyo na kuwasilisha michango toka wa wadau mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja Namba ya simu ya mama huyo tutaitoa kesho kwani sasa tunamshugulikia kupata namba yake ya simu maana hana kitambulisho chochote tunawasiliana na kijiji alikotoka watupatie barua ya kupeleaka katika makampuni ya simu asajiriwe Na Mbeya Yetu |
Wednesday, January 1, 2014
Tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu wa hali na mali mliotuonyesha kwa kipindi chote cha mwaka 2013.Ombi letu kwa Mungu mfanikiwe zaidi ili muendelee kuwa pamoja nasi kwa mwaka mpya 2014.
Heri,baraka,afya,utajiri na kila lililo jema na liwe kwenu nyote kwa mwaka 2014.
Asanteni Sana.
<<<<<Jerusalem Film Team>>>>>
Monday, December 30, 2013
Friday, December 27, 2013
Gari la kubebea wagonjwa 'ambulance' lililotolewa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa wananchi wa Buchosa.
Gari la kubebea wagonjwa 'ambulance' lililotolewa na Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa wananchi wa Buchosa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd wachapishaji wa magazeti ya Championi, Risasi, Ijumaa, Amani, Uwazi na Ijumaa Wikienda, Eric Shigongo, jana alikabidhi gari la kubebea wagonjwa 'ambulance' kwa Diwani wa Kata ya Bupandwa Mhela, Masumbuko Francis, ikiwa ni msaada kwa wakazi wa Buchosa. Pichani juu ni taswira za makabidhiano hayo yaliyofanyika jana katika sikukuu ya Krismasi huko Bupandwa Mhela, mkoani Mwanza.
(PICHA: CHANDE ABDALLAH NA DENIS MTIMA / GPL, MWANZA)
CHANZO: Global Publishers
Tuesday, December 24, 2013
Saturday, December 21, 2013
Hemed na mkewe siku ya ndoa yao huko Lusaka Zambia |
Kuona picha zaidi za yaliyojiri siku wawili hao waliposema 'I DO' gonga HAPA.
Video fupi ya tukio hili la kufurahisha itakujia hivi punde endelea kuperuzi blog hii inayokupa habari za kipekee kabisa ambazo huwezi pata sehemu nyingine!!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)